Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha leo imefanya hafla ya utoaji wa hundi ya mfano ya mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe. Hamoud Abuu Jumaa, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa mikopo hiyo, akibainisha kuwa ni chachu ya kuinua uchumi wa wananchi na maendeleo ya halmashauri.
Aidha, amewataka wataalam wa halmashauri kusimamia matumizi ya mikopo hiyo ili ilete tija.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Bi. Shukuru Lusanjala, amesema jumla ya vikundi 54 vitanufaika katika awamu ya kwanza, vikiwemo vikundi 34 vya wanawake, 13 vya vijana na 7 vya watu wenye ulemavu, hali itakayosaidia kupunguza changamoto ya ajira.
Hafla hiyo imehitimishwa kwa kukabidhi hundi ya mfano kwa vikundi vilivyonufaika.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

0 Comments