BWANKU AZUNGUKA SHULE KWA SHULE KUFUATILIA ZOEZI LA URIPOTI WANAFUNZI MASHULENI

Asisitiza walimu kupokea wanafunzi bila vikwazo vya sare, viatu kama alivyoelekeza Rais Samia ili kila Mtoto wa Kitanzania apate Elimu bila shida.

Tarafa ya Katerero ina shule 16 za Sekondari na Shule 55 za Msingi. Afisa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku leo Alhamisi Januari 22, 2026 ameendelea na ziara yake kuzunguka shule kwa shule ndani ya Kata zote 11 ndani ya Tarafa ili kukagua hali ya uripoti wa wanafunzi mashuleni kuanzia Darasa la Awali, Darasa la kwanza na Kidato cha kwanza.

Leo ziara yake imeendelea katika Kata ya Kemondo na Katerero ambako kote amepita madarasani kuona hali ya uripoti wa wanafunzi huku akisisitiza walimu kuendelea kupokea wanafunzi bila bughudha wala vikwazo vya aina yoyote ile ikiwemo sare, daftari n.k.

Afisa Tarafa Bwanku amesisitiza Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inatumia zaidi ya Bilioni 20 kwa mwezi kutoa Elimu bila malipo, kujenga Shule mpya kila mahali na kuweka mazingira bora ya Elimu nchi nzima ili kila Mtoto wa Kitanzania apate elimu.

Aidha, Bwanku ametumia wanafunzi hao kuwapa ujumbe wa kuwa mabalozi wa kwenda kuwapa ujumbe wanafunzi wenzao ambao bado hawajaripoti kuhakikisha wanaripoti haraka ili kuwahi masomo. 

Ziara hii ya Afisa Tarafa Bwanku itaendelea katika Kata zingine zote ambazo bado hajafika.





 

Post a Comment

0 Comments