DC MPOGOLO AUMALIZA MGOMO KIWANDA CHA NAMERA DAR.

 Na Moshi saidi

DAR-ES-SALAAM : MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemaliza mgomo wa wafanyakazi zaidi ya 1,500 wa Kiwanda cha Namera kilichopo Gongolamboto Dar es Salaam ulioanza Januari 16, mwaka huu.


Mgomo huo ulitokana na madai ya mishahara ambapo kima cha chini kwa sekta binafsi kimewekwa kwa mujibu wa Tangazo na Amri ya Serikali Namba 605A ya Oktoba 13, 2025, inayotoa ongezeko la wastani wa asilimia 33.4.

Kutokana na ongezeko hilo, mshahara wa chini umeongezeka kutoka Sh 275,060 mwaka 2022 hadi Sh 358,222 mwaka 2025. Mpogolo amesisiriza kuwa Amri ya Serikali ni lazima itekelezwe na kwamba hakuna kampuni, taasisi au mwajiri yeyote anayekubalika kushuka chini ya viwango vilivyowekwa kisheria.

Mpogolo ametoa maelekezo muhimu kwa uongozi wa kiwanda na wafanyakazi, ikiwemo kuhakikisha malipo ya mishahara yanatolewa kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 605A la mwaka 2025, huku akisisitiza kuwa hakuna mfanyakazi atakayefukuzwa kutokana na kushiriki mgomo ili kuimarisha mahusiano bora kati ya mwajiri na waajiriwa.

Aidha, ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi (TUICO) na Ofisa Kazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufanyika uchaguzi wa viongozi wa wafanyakazi watakao kuwa kiungo kati ya wafanyakazi na uongozi, pamoja na kupitia mikataba ya ajira kuhakikisha inakidhi sheria na kanuni zinazohitajika.

Post a Comment

0 Comments