Na Moshi saidi
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasan imekamilisha mradi wa Jengo la Viongozi Mashuhuri katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo la kisasa la Viongozi wa Kitaifa, Kimataifa na Wakuu wa Nchi (Presidential Pavilion), linatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 Januari, 2026 na Mheshimiwa Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof: Makame Mbarawa amesema Jengo hilo la kisasa lenye ghorofa moja linajumuisha kumbi tano (05) za Viongozi wa Kitaifa zikiwemo kumbi maalum mbili (Presidetial Suites); kumbi mbili za mikutano, ukumbi mmoja wa kusubiria (holding room), mgahawa n.k.
Amesema Hafla ya uzinduzi wa wa jengo Hilo ambalo Pia limefungwa mifumo ya kisasa ya umeme, maji, TEHAMA, Zimamoto, Viyoyozi (HVAC), usalama itaanza saa 2.00 kamili Asubuhi katika eneo la Terminal one katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Waziri Mbarawa ameeleza kuwa kwa sasa, Serikali inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato; Ukarabati na uboreshaji wa Viwanja vya Ndege vya JNIA, KIA, Shinyanga, Sumbawanga, Tabora, Kigoma, Lake Manyara, Tanga, Iringa na Musoma.


.jpeg)
.jpeg)

0 Comments