Algeria imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Congo DR katika mchezo wa AFCON 2025. Bao hilo la Algeria lilifungwa katika kipindi cha ziada.Mfungaji wa bao ni Adil Boulbina kutoka Algeria, ambaye alifunga bao la ushindi dakika ya 119, akimpeleka Algeria hatua ya robo faini ya AFCON 2025.
Algeria ilifuzu hatua ya 16 bora baada ya kumaliza nafasi ya kwanza katika Kundi E. Timu zilizofuzu kutoka Kundi E ni Algeria na Burkina Faso.
Algeria imewahi kutwaa ubingwa wa Afrika mara mbili, mwaka 1990 na 2019. Katika mashindano ya AFCON 2019, Algeria ilishinda fainali dhidi ya Senegal kwa bao 1-0, na kufanya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika Kaskazini kushinda ubingwa huo tangu 2004.

0 Comments