“Baada ya kurejea Algeria hatujapata muda mrefu sana wa kujiandaa. Safari ilikuwa ndefu sana. Tunayo changamoto ya kuhakikisha hatutoki nje ya mstari na malengo yetu. Sifa kubwa ya Yanga ni kushinda kila mechi. Haijalishi ni mashindano gani ila kipaumbele chetu ni kushinda mechi yetu ya Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate siku ya Alhamis”anasema Kocha Pedro.
“Tunafanya kazi kwa bidii kubwa mno kuhakikisha tunafanya vizuri na kusahihisha dosari ambazo zimejitokeza. Tunafahamu kuwa wapinzani wetu wamejiandaa vizuri pia. Tunahehsimu kila mpinzani anayekuja mbele yetu. Tutacheza kama vile tunacheza mchezo wa ligi ya Mabingwa. Falsafa yetu haitabadilka. Dhamira yetu ni ushindi tu”
“Tuna baadhi ya wachezaji ambao wanasumbuliwa na maumivu lakini na kuanzia leo nina matumaini. Naweza kusema nina asilimia kubwa ya kikosi ambacho nina kihitaji. Tunaendelea kufanyia kazi changamoto ndogo ndogo za majeraha kwa baadhi ya wachezaji ambazo zinawasumbua ili kuona utayari wao kimwili.

0 Comments