Home
About
Contact
Home
HABARI
MICHEZO
MAGAZETI
MAKALA
__DropDown 3
Home
TWENDENI HALE, TUKAPATE LADHA MPYA YA MSONDO NA SIKINDE
TWENDENI HALE, TUKAPATE LADHA MPYA YA MSONDO NA SIKINDE
Darasa Huru
December 21, 2025
NIMESOMA mtandaoni ujio wa onesho kubwa la dansi kwa ajili ya kuaga mwaka 2025.Ni lile litakalozikutanisha bendi kongwe za muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' na watani zao Mlimani Park Orchestra 'Sikinde Ngoma ya Ukae' litakalofanyika Desemba 26 mwaka huu Hale Lounge,Mkoani Tanga.Hakika Babu yenu Mzee Kionambali M.Kionambali nimevutiwa na ujio wa onesho hilo lenye sura na ladha tofauti na vile ambavyo tumezoea.Maonesho yenye kuzikutanisha bendi hizo yamezoeleka kufanyika jijini Dar es Salaam tu.
Bendi hizo hazijakutana nje ya Jiji la Dar es Salaam muda mrefu hivyo ni zilikuwa zinawanyima haki mashabiki wake waliojaa nchi nzima.Wajukuu zangu wa Hale wamefanikiwa kufanya mapinduzi ya kimuziki kwa kuleta burudani hiyo yenye sura ya kitaifa Mkoani Tanga.
Waandaji wameamua kubadilisha mandhari kutoka Dar es Salaam na sasa shughuli ya mtoto hatumwi dukani siku hiyo imeshushwa Mkoa wa waja leo waondoka leo.Hale ni pembezoni kidogo mwa Jiji la Tanga.Ni mji wenye mkusanyiko wa makabila mengi uliochangamka mno kibiashara sambamba na kujengeka kuendana na kasi ya maendeleo ya nchi.
Wajukuu zangu Hassan Msumari,Ally Kileo na wengine wanaoijua Hale ni mashuhuda wa sifa njema za mji huo wenye hali ya hewa ya kiubaridi tulivu.Hakika waandaji hawakukosea kuileta burudani hiyo Hale kutokana na mji huo kukidhi hadhi ya kupokea ugeni mkubwa wa wadau wa muziki wa dansi kutoka kila pembe ya nchi.
Hakika Hale ipo tayari kuwapokea mashabiki wa Msondo na Sikinde kwa mara ya kwanza katika jukwaa moja.Naifahamu vyema Hale kwakuwa Babu yenu Kionambali mke wangu wanne(yaani bibi yenu) anatoka hapo na nilifunga naye ndoa mwaka 1988.
Unaweza kuona umbali wa kutoka kijijini kwangu Kisiju, Mkuranga, Pwani hadi kuja kuopoa chombo Hale.Licha mandhari nzuri ya mji huo pia umejaaliwa kumiliki hazina ya mabinti warembo haswa.Kwa wajukuu zangu vijana kwao ni fursa adhimu ya kutakasa macho kabla ya kusogelea lengo la kuachana na ukapera. Naam hakika Hale imejaaliwa neema nyingi zinazoweza kukufanya ukaloea baada ya onesho hilo na kujikuta ukifanya Utalii wa ndani.
Babu yenu nimeanza kudunduliza fedha mpaka Desemba 25 niwe Hale tayari kwa kushuhudia burudani ya Msondo na Sikinde nje ya viwanja vyao vya nyumbani.Kwa bahati nzuri onesho hili limekuja msimu wa mavuno huku Kisiju kwahiyo fedha ya malazi na chakula kwangu haiwezi kuwa shida.
Siwezi kuiacha burudani ya Msondo na Sikinde nje ya Jiji la Dar es Salaam inipite kirahisi.Licha ya uzee wangu wa miaka(87)nilionao lakini nasema nitajikongoja kwenda Hale siyo kwa ajili ya kwenda kuwasalimia wakwe zangu bali ile burudani ya Msondo na Sikinde ndiyo itakayonipeleka huko.
Nitashangaa kuona wewe mdau wa muziki wa dansi unaachaje kufunga mwaka na shoo yenye ladha mpyaTwendeni Hale wajukuu zangu tukapate burudani ya muziki wa dansi sambamba na kujionea mandhari nzuri ya mji huo.Nimesikia taarifa zisizo rasmi baadhi ya wajumbe wa Kamati za Ufundi wa bendi hizo tayari wako Hale wakipita maeneo mbalimbali kuweka mambo sawa maana inaelezwa kila mmoja amepania kumtoa nishai mwenzie jukwaani.
Kionambali M.Kionambali
S.L.P 2785
0754-629298
Kisiju/Mkuranga Pwani
21/12/2025
Post a Comment
0 Comments
Social Plugin
ZILIZOSOMWA ZAIDI
TFF WATOA TAREHE RASMI YA TUZO ZA WACHEZAJI BORA NBC 2024-25
November 14, 2025
HAYA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2025
January 10, 2026
KIKOSI CHA YANGA SC DHIDI YA SINGIDA BLACK STARS HIKI HAPA
January 09, 2026
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2025
January 10, 2026
RAIS SAMIA AAGIZA VIJANA WALIOFUATA MKUMBO OKTOBA 29 WAACHIWE
November 14, 2025
TUTAZAME YOUTUBE
0 Comments