SIMULIZI KUTOKA BAGAMOYO

 


(Mwache Apotee)
Mtunzi Jimmy Chika
0712328223

*MWANZO*

Sikuwa nikiwafahamu wazazi wangu, lakini simulizi za wazee wananiambia nimeishi kwa kulelewa na wasamalia tofauti.

Wananiambia kuna wawindaji walioniokota msituni wakiwa katika hrakati za mawindo.

Wakanipa majina mengi lakini hili linalovuma kwa sasa nikiwa na fahamu wananiita Mwache Apotee.

Jina hili naambiwa lilikuja kutokana na tabia yangi tangu nilipookotwa nikiwa na miaka mitatu.

Wanasema mara nyingi wawindaji wanaponisaidia kunipa chakula na maji na kuniweka katika mabanda yao ya kuanika nyama ghafla nilikuwa nikitoroka.

Pengine nilimaliza hadi saa tatu msituni bila kuonekana pale kibandani.

Tabia hii ikawachosha wawindaji hivyo wakawa wanasema "Huyu mtoto mtundu sana, Mwache apotee" jina hili likazoeleka.

Hata sasa nikiwa mtu mzima naendelea kutumia jina hilo.

Kipaji kikubwa alichonishushia Mungu ghafla ni uwezo mkubwa wa kuendesha majahazi pia kuyafanyia ukarafati.

Kadri nilivyokuwa nikifanya kazi hii pia nikiishi katika kijiji cha Utondwe karibu na mji wa kale wa Saadani nilikuwa nikijiuliza juu ya ukoo wangu.

Wazee wote niliokuwa nikiishi nao hapa wakifanya kazi ya uvuvi na wengine wakikata ukindu walikuwa wakijitaja kwa majina mawili lakini mimi nikabaki na jina hilohilo moja tu Mwache Apotee.

Kuna wakati hawa wazee walikuwa wakinifananisha na koo fulani lakini hakukuwa na mwenye majibu ya uhakika kuhusu ukoo wangu.

Japo niliumia sana moyoni lakini haikunizuia kuendelea na shughuli zangu katika majahazi.

Ajabu katika kazi hii nikapata umaarufu uliosambaa katika ukanda wote wa vijiji vya Mwambao.
.
Ukianzia hapa Utondwe hadi Gama na huku viijiji vya Uvinje, Buyuni Kitopeni, Buyuni Kuu, Sakura, Mwela hadi Pangani hakuna mvuvi atakayeunda jahazi au kidau bila kuniita kwa ajili ya kuziba nyufa, tunaita kukarafati.

Moyoni mwangu nikawa na siri kubwa ya kumiliki pesa nyingi nilizozifukia katika chungu chini ya uvungu wa kitanda changu kilichopo katika banda langu hapa kijijini Utondwe.

Kwa bahati nzuri hapa kijijini naweza kusema banda langu ndiyo imara zaidi nimelijenga kwa smenti nyingi paa lake ni refu sana kuliko ukuta wa matofali hivyo muonekano umekuwa kama vile bati zinakaribia kugusa chini.

Mita 50 banda langu nimezungusha wigo si rahisi mtu kuingia lazima apige hodi kutoka mbali ndiyo nikanfungulie.

Japokuwa hapa kijijini kuna nyumba kama nne zinazowaka taa za Sola usiku lakini taa zangu ni tofauti kabisa.

Niliagiza vyuma virefu vinavyofanana na zile taa za Sola za Tanga zinazofungwa barabarani.

Hivyo hata ukiwa mbali na kijiji hiki cha Utondwe wakati wa usiku utaziona taa hizi.

Zimekuwa msaada hata kwa kijiji maana zamani wanyama ka Simba au viboko walikuwa wakiingia kijijini na kujeruhi watu.

Kwa kuwa pesa yangu haikuwa na matumizi niliweza kununua ninachotaka mara nyingi nikijifungia ndani na kuzihesabu kisha nikiwapeleleza watu waliosoma wanaokuja kununua samaki nikagundua kuwa naweza hata kununua gari au Trekta lakini sikutaka kufanya hivyo.

Kwa kuwa mwenyewe ni mjuzi naweza kuunda boti ukadhani imetoka Ulaya kilichonishinda ni kupulizia rangi.

Hiyo ndiyo gharama iliyogusa kidogo sana akina yangu maana niliagiza wataalam wa kupaka rangi kufunga vioo na kuweka usukani kama wa gari na kufungq viti vya masofa kwenye boti yangu.

Nilitaka iwe nzuri kuliko zile zinazobeba watalii ninazopishana nazo mara kwa mara baharini.

Japokuwa sikuwa na elimu lakini nashukuru niliwasumbua watu hapa kijijini hata kwa kuwalipa mpaka sasa najua kusoma hata gazeti.

Kwa hiyo nilimalizana na mafundi walipomaliza kuandika jina langu Mwache Apotee pembeni ya mlango.

Kwa vile mafuta ya kuendeshea injini ya boti yangu yalipatikana mbali nikaamua kununua pipa zima nikahifadhi kando ya banda langu ninalofugia ndege.

Nikajiwekea mazoea kama siku nikiwa sina kazi huwa nawasha boti yangu na kutembea tu katika vijiji mbalimba na hata siku nyingine nikipiga hodi visiwa vya Tumbatu Unguja huko kulikuwa na rafiki zangu wawili wavuvi.

Nakumbuka kuna siku nilitamani kupumzika nikapanga nijiandae kutoka.

Huwa nikiwa na siku kama hizo huwa naamua kama nitapenda kula kuku au ndege au samaki basi huwa nandaa chakula changu usiku.

Siku hiyo nikatamani nile aamaki wa kuchoma lakini awe mkubwa.

Ilikuwa kazi ndogo sana nikawasha boti yangu nikaenda katika kina kirefu bahari ilikuwa shwari kabisa nikazima mashine ya boti nikatia nanga boti ikawa imesimama.

Nikatupa ndoano baharini hata dakika 10 hazikufika nikamnasa samaki mkubwa aina ya Mkizi anayefika kama kilo tano hivi.

Nikaona huyu anafaa kwa sherehe yangu na mwingine atabaki nitawala wavuvi kesho wanaopenda kunywa chai na mihogo na samaki. Itaendelea Jumatano....

Post a Comment

0 Comments