Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam yametangazwa rasmi leo, yakionesha ushindani mkali kati ya wagombea wanne waliowania nafasi hiyo. Uchaguzi huo umefanyika kwa utulivu huku wajumbe wa Baraza la Jiji wakipiga kura kuamua uongozi mpya wa jiji hilo muhimu nchini.
Katika matokeo yaliyotangazwa, Nurlin Djuma maarufu Sheta ameibuka kidedea baada ya kupata kura 25, akifuatiwa kwa karibu na Robert J. Manangwa aliyepata 23. Wagombea wengine ni Saddy Mohamed Kimizi aliyepata 7, na aliyekuwa anatetea kiti hicho, Omary Saidi Kumbilamoto, aliyepata 4. Kura 6 zimeripotiwa kuharibika.
Kwa ushindi huo, Shetta ameandika historia ya kuliongoza Jiji la Dar es Salaam, huku akimuangusha aliyekuwa Meya, Mh. Kumbilamoto. Wananchi na wadau wa maendeleo ya jiji wanatarajiwa kufuatilia kwa karibu hatua na mitazamo mipya ambayo uongozi huu mpya utaleta katika kuboresha huduma na ustawi wa Dar es Salaam.


.jpeg)
0 Comments