Rebeiro atajwa Kuinoa Simba SC

Klabu ya Simba SC imeelekeza macho yake kwa kocha José Rebeiro, ambaye sasa anatajwa kuwa chaguo namba moja kuinoa kikosi hicho kikongwe cha Tanzania.
 Rebeiro, ambaye amewahi kuvichezea na kuvifundisha vilabu vikubwa barani Afrika kama Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Al Ahly ya Misri, ameonyesha uwezo mkubwa wa kiufundi na kuacha alama kila alikopita.

Kwa sasa, Simba SC inasaka kocha mwenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa, na jina la Rebeiro limeibuka kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa kuchukua mikoba ya benchi la ufundi.

Taarifa zinaeleza kuwa Simba haitaki tena unyonge wala majaribio, na safari hii wanataka kocha mwenye rekodi ya ushindi na nidhamu ya hali ya juu kuiongoza timu hiyo kufikia mafanikio ya Afrika.

Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwa sasa wanasubiri kwa hamu kuthibitishwa kwa dili hilo ambalo huenda likabadili kabisa mwelekeo wa timu hiyo.


Post a Comment

0 Comments