MZIZE, YAO KOUASSI KUREJEA UWANJANI MWAKANI

Mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Clement Mzize 🇹🇿 pamoja na Beki wa kulia wa Klabu hiyo, Yao Kouassi wanatarajia kurejea rasmi uwanjani kucheza mechi za Kimashindano mwishoni mwa Mwezi January au Mwanzoni mwa Mwezi Februari ambapo watakuwa wamepona kwa asilimia 100 tayari kwa kuwatumikia Wananchi. 

.
Kwenye taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema wachezaji hao kwa sasa wanaendelea vizuri na wataanza kucheza mechi za kimashindano Ligi itakaporejea mara baada ya Michuano ya AFCON.
.
Kwa upande wa Mudathir Yahya, Ally Kamwe amesema kiungo huyo anaendelea na matibabu ambapo kwa mjibu wa madaktari kiungo huyo atakuwa tayari kucheza mwanzoni mwa mwezi January

Post a Comment

0 Comments