Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amewataka vijana nchini kuendelea kudumisha utulivu na kutii sheria, hasa kipindi hiki kinapoelekea tarehe 9 Desemba.
Akiwa na waandishi wa habari leo, Msama amesema wazazi na walezi wanalo jukumu kubwa la kuwasimamia watoto wao na kuwatahadharisha dhidi ya misukumo inayoweza kuwaingiza kwenye matatizo. Ameeleza kuwa usimamizi wa familia ni msingi muhimu wa kulinda amani katika jamii.
Katika maelezo yake, Msama amewahimiza viongozi wa dini kuendeleza elimu kuhusu umuhimu wa kutetea amani, akisema vijana wanapaswa kusikiliza maongozi ya kiroho yanayolenga kujenga jamii tulivu.
Amesisitiza pia kuwa wanaharakati wa haki za binadamu wana nafasi muhimu ya kuelekeza jamii kuheshimu misingi ya kisheria, kwani hakuna haki inayoweza kutetea nje ya mazingira ya amani na sheria.

0 Comments