Chama Cha Mapinduzi kimesema kwa
kile kinachopitiwa na Tanzania wakati huu hakikuanza jana ,juzi au
Mwezi uliopita bali ni mapambano ya kiuchumi baada ya Ardhi yake
kugundulika Madini adimu duniani.
CCM kimesema huenda wakajitokeza maadui zaidi watakaotumiwa kama njia ya kufanikisha mkakati wa kuhatarishaa Amani endapo Watanzania watagawanyika.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar , Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis ameeleza ameyaasa Mataifa makubwa yaache kutoa visingizio vya kudhoofu kwa domokrasia au kutaja chaguzi kuu hazikuwa huru.
Mbeto alisema Duniani kumeibuka Vita ya Kiuchumi iliojaa hila na ghilba zitokanazo na uchu wa kuhodhi Madini adim yanayohitajiwa kwa Maendeleo ya Mataifa makubwa.
Alisesma hadithi au simulizi za kuipa majina mabaya Tanzania na vitisho yabis , zilianza kwa kudai kuna uongozi wa kidikteta , ukandamizaji haki , demokrasia , Uhuru wa vyombo vya habari na kilichoitwa kifo cha Upinzani.
" Hizi zote ni hadithi za ubabaifu .Miradi miwili ya Uranium ya Mkuju na
Liganga imefumua joto la taharuki duniani. Wakati Mkuju si mgodi tu wa Uranium bali pia ni mojawapo ya maeneo muhimu Duniani" Alisema Mbeto
Alisema hatua ya Shirika la Nyuklia la Urusi kuchukua Mradi wa Nyuklia , ndio mwanzo wa kuzuka fitna nyeusi baada ya Tanzania na Urusi kuzindua Kiwanda cha majaribio cha usindikaji wa Uranium Mkuju.
Alisema kwa Mradi wa Lindi Liganga ,
Kampuni za Magharibi toka Mwaka 2018–2023 zilijadiliana bila mafanikio huku China , Falme za Kiarabu na Gazprom ya Urusi, zikionyesha nia ya kuanza kushiriki.
"Taswira iliopo ni Uranium kwenda Urusi Gesi itahodhiwa na China , Nchi za Gulf , Urusi huku nchi za Magharibi zikitaka kujua endapo hakutakuwa na mabadiliko yoyote " Alieleza
Mbeto alisema hapo ndipo ilipoanza vita ya kidijitali kwani kama inavyojulikana siku hizi vita haipiganwi kwa bunduki bali kwa matumizi ya mitandao ya kijamii .
"Tanzania haitapuuza msimamo wake wa kujadiliana na kiungwana ili kufikia makubaliano ya kiungwana. Vitisho na propaganda uchwara lazima zikomeshwe . Madai ya udhaifu wa demokrasia , chaguzi kutokuwa huru au ukandamizaji wa aina yoyote zikome "Alieleza
Hata hivyo, Katibu huyo Mwenezi alisema Tanzania haitabaki peke yake, badala yake itashirikiana na Dunia ili kulinda Utu na maslahi yake na kuyapa indhar Mataifa kadhaa yaache kutumia mradi wa udini, ukabila na kupandikiza mamluki.

0 Comments