MAMBA MSUMBUFU AUWAWA MTO RUVU, KIBAHA DC.
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha imefanikiwa kudhibiti mamba mmoja hatarishi kati ya mamba watatu waliokuwa wakihatarisha maisha ya wananchi na mifugo katika Kata ya Mtambani, Kitongoji cha Miandebomu kando ya Mto Ruvu.
Wataalam wa wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Lameck Makuwe, Leonard Haule na Peter Kisaka, walisema kuwa zoezi la kuwasaka mamba wawili waliobaki bado linaendelea mchana na usiku ili kulinda usalama wa wananchi na mifugo yao.
Mamba huyo aliyedhibitiwa alikuwa na urefu wa futi 9–10, na kuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli za kila siku za wananchi.
Maafisa wanyamapori wameendelea kutoa elimu juu ya kujilinda dhidi ya wanyama wakali.
"Wananchi wanapaswa kuishi kwa makubaliano na mazingira huku wakiendelea kuzingatia maelekezo ya usalama yanayotolewa mara kwa mara" Maafisa wanyama pori.
Aidha, namba za mawasiliano za maafisa wanayama pori zimetolewa ili kurahisisha kuripoti hali hatarishi kwa wakati.
Wananchi wa vitongoji husika waliishukuru Serikali kwa kuwaletea maafisa wanyamapori, jambo lililowasaidia kupata elimu muhimu juu ya usalama wao.
Maafisa wanyamapori wamewahimiza wananchi kutoa taarifa mara moja pindi wanapokumbana na wanyama hao hatarishi ili hatua za haraka zichukuliwe.

0 Comments