Suala la Thadei Kweka lafichua hatari ya watu walioukana uraia kuingilia masuala ya ndani ya Taifa.
Taarifa
iliyotolewa na Malisa Godlisten akidhani analichafua jeshi la polisi
kumkata Mtanzania aliyeukana utanzania na kuwa mmarekani Thadei Kweka
imeweka wazi ukweli mzito unaopaswa kuangaliwa kwa jicho la Taifa kuwa
watu wanaohamasisha vurugu,uchochezi na uvunjifu wa amani si Watanzania,
na hata watanzania wachache hawaishi Tanzania kama inavyozidi
kubainika
Kwa mujibu wa
taarifa ya Malisa , Thadei Kweka anayetajwa katika sakata hilo sio raia
wa Tanzania, bali ni raia wa Marekani aliyeukana uraia wa Tanzania, na
aliingia nchini kwa Tourist Visa ya muda wa siku 90.
Huu
ni uthibitisho wa wazi kwamba mhusika hakuwa nchini kama Mtanzania,
bali kama mgeni ambaye kipindi akiwa marekani alikuwa anatukana
serikali, anashawishi vurugu na uchochezi huku watanzania hasa vijana
wakijua ni mwenzao .
Kukana Uraia ni Kukana Taifa
Ifahamike
kuwa Uraia wa nchi si hati ya kusafiria pekee, bali ni Kiapo cha utii
kwa Taifa, Ahadi ya kulinda amani na mshikamano na Msingi wa mapenzi ya
dhati kwa nchi
Mtu
anapoukana uraia wa Tanzania, kwa mantiki hiyo anaukana Utii kwa mamlaka
ya nchi, Wajibu wa kulinda amani ya Taifa, Maadili na misingi ya utaifa
na kupoteza sifa na hazi zote za watanzania
Haiwezekani
mtu aliyelikataa Taifa abaki na madai ya kulipangia wake, hususan kwa
njia zinazohatarisha amani na usalama wa nchi.
Taarifa
ya Malisa inaonesha pia kuwa hata taratibu za kidiplomasia
zilihusishwa, ikiwemo kuwasiliana na ubalozi wa Marekani, jambo
linalozidi kuthibitisha kuwa anayezungumziwa hakuwa Mtanzania, bali raia
wa nchi nyingine.
Watanzania wa Kweli Wanachagua Amani
Historia
na uhalisia wa Tanzania unaonesha kuwa Watanzania wanapotofautiana,
hutumia njia za kikatiba, Wanapodai haki, hutanguliza amani na utulivu,
Hawachochei machafuko yanayohatarisha maisha, mali na mustakabali wa
Taifa
Ni dhahiri kuwa
vurugu nyingi hazichochewi na Watanzania halisi, bali na watu waliokata
mizizi yao ya utaifa, au wasiokuwa na dhamira ya kweli kwa mustakabali
wa nchi.
Kwa msingi wa
taarifa ya Malisa Godlisten, hoja ni wazi kuwa watu waliokata tamaa,
wakaukana uraia wa Tanzania, hawawezi kuwa na mapenzi ya Taifa.
Na
pale watu wa aina hiyo wanapojaribu kuingilia masuala ya ndani ya nchi,
Taifa lina wajibu wa kusimama imara kulinda amani, mamlaka na heshima
ya Tanzania.
Habibu Mchange
Mwenyekiti-MECIRA

0 Comments