MSANII WA SINGELI MAMA AMINA AITWA BASATA KISA HIKI HAPA

Msanii wa Singeli, Mama Amina, akiwa pamoja na timu yake ya usimamizi @pachekomidundo amefika katika Ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akiwa ameitikia wito wa Baraza.

Ziara hiyo imelenga kumpa elimu kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili katika utayarishaji na utoaji wa kazi za sanaa, sambamba na kukamilisha taratibu za usajili wake BASATA.

BASATA imeendelea kutoa wito kwa wasanii wote nchini kuhakikisha wanazingatia sheria, maadili na kanuni zinazoongoza sekta ya sanaa, kwa manufaa ya kukuza ubora wa kazi zao na kulinda taswira njema ya sanaa ya Tanzania.


 

Post a Comment

0 Comments