Rais Dkt Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 16 OKTOBA 2025 alipozungumza katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Uwanja waMichezo wa Paje,Mkoa wa Kusini Unguja.
Ameeleza Mradi mwengine ni Ujenzi wa Madaraja kwa ajili ya kuiunganisha Mkoa ya Kusini na Kaskazini Unguja kwa Ujenzi wa Daraja la Unguja Ukuu- Uzi Ng'ambwa unaoendelea pamoja na Ujenzi wa daraja la Chwaka hadi Charawe.
Dkt Mwinyi amewahakikishia Wananchi Ujenzi wa Bandari ya Kizimkazi pamoja na kuziimrisha Bandari Ndogo za Mtene,Chwaka naUnguja Ukuu na Ujenzi wa Kiwanja Cha Ndege cha Nungwi na Kiwanja Cha Paje na kuelezea kuwa Kukamilika kwa miradi hiyo kutaufungua Mkoa wa Kusini Kiuchumi na Ustawi wa Jamii.
Rais Dkt, Mwinyi amesema Serikqli itajenga madarasa mapya katika Mkoa wa kusini ikiwemo Madarasa 1000 kwa Skuli za Msingi na mengine 1000 kwa skuli za Sekondari utakaombatana na skuli za Msingi 4 na Skuli 10 za Sekondari zote zikiwa za ghorofa.
Akizungumzia sekta ya Afya amesema Serikali inajipanga kujenga Hospitali ya Mkoa wa Kusini Unguja wakati tayari ikiendelea na Ujenzi wa Hosptali ya Rufaa ya kufundishia ya Binguni na Hospitali Kutibu Saratani ya Binguni,,kuhusiana na suala la Maji ameeleza kuwa Serikali inajipanga kutekeleza Mradi mkubwa wa Maji katika Mkoa huo utakaogharimu Dola za Marekani Milioni 55, Mradi utakaomaliza tatizo la Maji Mkoani humo.
Ameyataja maeneo yatakayonufaika na Mradi huo kuwa ni Uroa, Marumbi ,Pongwe, Jambiani na Makunduchi
Eneo jengine ni kuwawezesha Wanachi Kiuchumi kwa kuwapatia Mafunzo ,Vifaa vya Kutendea Kazi , Mikopo isio na Riba na kuwawekea Mazingira Bora ya kufanyia kazi zao kwa Wajasiriamali.
Rais Dkt, Mwinyi ameendeleza kuwahimiza Wananchi Umuhmu wa Kudumisha Amani wakati huu kuelekea Uchaguzi na Baada ya Uchaguzi kwani ndio nyenzo muhimu ilioiwezesha Serikali kutekeleza Miradi mingi ya Maendeleo katika Miaka Minne iliopita.
Mgombea huyo wa Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar amewaomba Wananchi Kumchagua tena kuiongoza Zanzibar ili aendelee kuleta Maendeleo Makubwa zaidi chini ya Kaulimbiu yake ya "YAJAYO NI NEEMA ZAIDI"
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dkt, Muhammed Said Dimwa amemuelezea Dkt, Mwinyi kuwa Kiongozi Muadilifu,Mkweli na mwenye Hekima katika Utendaji wake na kuwaomba Wananchi kumchagua tena kuiongoza Zanzibar kwa mafanikio zaidi
Tags
Habari
.jpeg)