Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar , Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi leo tarehe 8 Septemba 2025 amekutana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Asha Rose Migiro, Ikulu Zanzibar.
Dkt.
Mwinyi amempongeza Dkt.Migiro kwa uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu CCM
Taifa na kueleza matumaini yake makubwa kutokana na uwezo wake, huku
akifurahishwa na mwenendo wa kampeni za CCM unaoashiria kukubalika kwa
Chama na ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Aidha, amemtakia
mafanikio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM , Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, na kushukuru CCM Makao Makuu kwa msaada wake kuelekea uzinduzi
wa Kampeni Zanzibar Septemba 13.
Naye, Katibu Mkuu Dkt. Migiro ameahidi kushirikiana na CCM Zanzibar na kufanya kazi bega kwa bega katika kampeni.