Baada ya kukamilisha ziara ya mtaa kwa mtaa kwenye kata ya Tambuka Reli,Tarehe 11.09.2025 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba kwa tiketi ya CCM Ndg. Anthony Mavunde amefanya mkutano wa hadhara wa wananchi na kuwasilisha mambo yafuatayo;
▪️Usimamizi wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika kujibu changamoto za wananchi.
▪️Ukamilishwaji wa ujenzi wa zahanati-Chadulu
▪️Mikopo ya wakina mama,vijana na wenye ulemavu
▪️Ukarabati wa miundombinu ya Majitaka
▪️Ujenzi wa uzio wa Shule ya Msingi Chadulu
▪️Ukarabati mkubwa wa barabara ya Morena-Chadulu
▪️Utatuzi wa migogoro ya Ardhi
▪️Ukamilishwaji wa ujenzi wa Kivuko cha Sekondari ya Sechelela
▪️Kuboresha miundombinu ya Shule ya Msingi Dodoma Mlimani
▪️Ujenzi wa Ofisi ya Mtaa wa Salmin
▪️Kukamilika kwa Ujenzi wa Soko la Chadulu
▪️Ujenzi wa Kituo cha Polisi.