Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutoa huduma katika
Maonesho ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayoendelea
viwanja vya Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katika maonesho
hayo yaliyobeba kaulimbiu ya "Fahari ya Tanzania" Wizara ya Ardhi natoa
baadhi ya huduma kama vile Hati Milki za Ardhi kwa aliyekamilisha
taratibu za umiliki, Ubadilishaji jina (Deed poll), Ukadiriaji Kodi ya
Pango la Ardhi, Uthamini wa Mali zinazihamishika na zile zisizohamishika
pamoja na utatuzi wa changamoto za sekta ya ardhi.
Aidha,
huduma za sekta ya Ardhi katika manispaa za mkoa wa Dar es salaam
Kinondoni, Ubungo, Kigamboni, Ilala, Temeke pamoja na Mabaraza ya Ardhi
na Nyumba ya Wilaya zinapatikana katika banda la Wizara.
Vile
vile, elimu kuhusiana na masula ya sekta ya milki, urasimishaji pamoja
na namna ya kujiunga na Chuo cha Ardhi Morogoro (ARIMO) katika masomo
kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada inatolewa na wataalamu sambamba
na kutoa fomu za kujiunga na chuo hicho.