Rais William Ruto ametangaza rasmi uteuzi wa Mwenyekiti na Makamishna wapya wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Hatua hiyo inafuatia uamuzi uliotolewa na majaji watatu uliotupilia mbali ombi la kupinga uteuzi huo ambalo lilihoji uwezo wao
Tangazo
katika Gazeti la serikali namba 9269, ya Julai 10, 2025, Ruto alimteua
Erastus Edung Ethekon kuwa Mwenyekiti mpya wa IEBC kwa muhula wa miaka
sita.
Katika tangazo tofauti la Gazeti la serikali Namba 9270,
pia lililotolewa Julai 10, 2025, Ruto alitaja watu sita kuhudumu kama
makamishna wa IEBC kwa kipindi kama hicho cha miaka sita.
Wateule
ni Ann Njeri Nderitu, Moses Alutalala Mukhwana, Mary Karen Sorobit,
Hassan Noor Hassan, Francis Odhiambo Aduol, na Fahima Araphat Abdallah.
Mahakama
Kuu ilisema wakati uteuzi wenyewe ulikuwa halali, ilani ya awali ya
Gazeti iliyotolewa na Rais ilikuwa imechapishwa kwa kukiuka amri ya
mahakama.
Matokeo yake, Notisi ya awali ya Gazeti ilitupiliwa mbali, na kuhitaji kuchapishwa upya kulingana na uamuzi wa mahakama.
Kwa
matangazo mapya katika Gazeti rasmi la serikali, Mwenyekiti na
Makamishna wanatarajiwa kula kiapo mbele ya Jaji Mkuu, ili kuanza rasmi
majukumu yao katika Tume ya Uchaguzi.
