WAZIRI KATAMBI AWAITA MABAUNSA,SHEIKH MWAIPOPO

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewataka viongozi wa makundi mbalimbali kufika katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam kesho, Septemba 4, 2026, kwa ajili ya kikao maalum.
Miongoni mwa waliotakiwa kufika ni Sheikh Said Mwaipopo pamoja na kundi lake la mabaunsa, viongozi wa vikundi mbalimbali vya mabaunsa, pamoja na Mwenyekiti na Katibu wa Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi.
 
Kwa mujibu wa wito huo, makundi hayo yametakiwa kufika katika Wizara hiyo saa 3:00 asubuhi.
Wakati huohuo, Waziri Katambi ametoa wito mwingine kwa wasanii na watu maarufu mitandaoni ambao hawakuitikia wito wa awali uliotolewa kwa ajili ya kufika Wizara hiyo tarehe Septemba 2, 2026.
 
Watu hao wametakiwa kufika bila kukosa kesho, Septemba 4, 2026, katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Waliotajwa katika wito huo ni Jenifer Jovin maarufu Niffer, Godfrey Tumaini anayefahamika kama Dudubaya, Nasma Hassan Athuman maarufu Nana Dolls, pamoja na Twalib Bakari Mungiya anayefahamika kama Uncle T.
 
Wanne hao wametakiwa kufika katika Wizara hiyo saa 4:00 asubuhi.
Wito huo umeweka mkazo kwa makundi hayo kufika kwa wakati uliopangwa, huku hatua zaidi zikitarajiwa kufahamika baada ya kikao hicho.

Post a Comment

0 Comments