UTAPELI MTANDAONI KATAMBI AYAITA MAKAMPUNI YA SIMU

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameitisha kikao na kampuni za simu nchini ikiwemo Vodacom, Airtel, Yas, Halotel na TTCL, kujadili namna ya kukabiliana na kuongezeka kwa uhalifu wa mitandaoni unaotumia namba za simu.

Kikao hicho kinatarajiwa kujadili kwa kina mbinu za kukabiliana na utapeli unaofanywa kupitia simu, ikiwemo matukio ambapo wahalifu huwapigia wazazi au ndugu na kujifanya kuwa mtoto wao anaumwa au amepatwa na tatizo, kisha kuwaomba watume fedha kwa dharura.

Waziri Katambi ametoa wito kwa kampuni hizo kufika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam, Septemba 4, 2026 saa 7:00 mchana, kwa ajili ya kikao hicho.

Hatua hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na kampuni za mawasiliano katika kudhibiti matumizi mabaya ya namba za simu, kubaini wahalifu na kulinda wananchi dhidi ya utapeli wa mitandaoni.

Post a Comment

0 Comments