Takriban watu 46 wamefariki dunia katika jimbo la Sokoto, Kaskazini-Magharibi mwa nchi ya Nigeria baada ya boti kuzama.
Maafisa wanasema boti hiyo ilibeba zaidi ya watu 70, wengi wao wakiwa watoto, ambapo bado operesheni ya uokoaji inaendelea.
Msemaji wa Polisi, Ahmad Rufai, amesema kuwa miili 46 imepatikana karibu na Gorau katika eneo la Gorony.
Rufai
ameongeza kuwa watu 16 wameokolewa, huku 15 wakiwa bado hawajapatikana
na kueleza kuwa eneo hilo ni gumu kufikika, na vyombo vya usalama pamoja
na huduma za dharura vinaelekea eneo la tukio.
Shuhuda mmoja
aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa anaamini watoto waliokuwemo
ndani ya boti hiyo walikuwa wakisafiri na wamiliki wa mashamba pamoja
na vibarua waliokuwa wakielekea kufanya kazi ya kuvuna mpunga.
0 Comments