Jeshi la
Polisi nchini limetolea ufafanuzi picha mjongeo inayosambazwa kwenye
mitandao ya kijamii ikionesha Dereva wa Pikipiki akizozana na Askari
Polisi huku askari hao wakijitahidi kuyaondoa barabarani magunia ya
alizeti aliyokuwa amebeba dereva huyo kwenye pikipiki.
Tukio hilo lilitokea Julai 30,2026 Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.
Askari
hao walikuwa wanapitisha msafara wa Mwenge wa Uhuru ndipo Dereva huyo
wa pikipiki alisimamishwa kwa ajili ya usalama wake na wa watu wengine
làkini alikaidi ndipo ikabidi Askari wamzuie na matokeo yake pikipiki
ikadondoka.
Polisi wamesema tukio hilo lilianza kushughulikiwa na
kuchukuwa hatua kuanzia hiyo Julai 30,2026 ikiwa ni pamoja na kupata
maelezo sahihi ya walioshuhudia kilichotokea toka mwanzo.
Jeshi
la Polisi linaendelea kutoa wito kwa kila mmoja kutii sheria na kufuata
maelekezo ya kiusalama yanayotolewa kwa ajili ya usalama wetu ili
kuepuka madhara na migongano isiyo ya lazima.
0 Comments