Boksi ambalo
bado halijafahamika lina nini ndani yake limekutwa Kituo cha Mabasi cha
kwenda Tegeta maeneo ya Mwenge, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa mtaa
wa Mlalakuwa, Suleiman Masare amesema kuwa boksi hilo lilitelekezwa
tangu jioni ya jana Jumatano Agosti 5,2026.
Masare amesema boksi
hilo limezua taharuki kwa wananchi, huku Jeshi la Polisi likianza
taratibu za kulikagua na kulifungua ili kubaini kilichomo ndani na
kuondoa hofu iliyojitokeza.
Jeshi la Polisi limechukua boksi lililokuwa limetelekezwa eneo la Mwenge, Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi.
Boksi hilo limepelekwa Kituo cha Polisi Mabatini, Kijitonyama, ambako taratibu za uchunguzi zinaendelea.
Jeshi
la Polisi limesema taarifa kamili kuhusu kilichomo ndani ya boksi hilo
itatolewa kwa umma baada ya uchunguzi na kulifungua kukamilika.
0 Comments