SIMBA SC WAUTEKA MSIMAMO WA LIGI KUU NBC

 Imeandikwa na Ally Mandai.

Mnyama, Simba SC imeendeleza mwanzo mzuri wa msimu wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo uliochezwa leo kwenye dimba la Airtel, Singida.

GUSA HAPA,UREJESHE HESHIMA CHUMBANI NA TIBA LISHE 

Simba ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya 12 kupitia Clatous Chama, kabla ya Singida Black Stars kusawazisha dakika ya 22 kupitia Sheikhan, na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.

 

Kipindi cha pili Simba ilirejea ikiwa na nguvu zaidi na kupata bao la pili dakika ya 62 kupitia De Reuck, aliyefunga kwa mkwaju wa penalti na kuipa Simba uongozi wa mabao 2-1.

Hata hivyo, dakika ya 85, Simba ililazimika kumaliza mchezo ikiwa pungufu baada ya beki wake wa kushoto, Anthony Mligo, kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia rafu mbaya. Hilo limeifanya Simba kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 uwanjani.

Kadi hiyo imeendeleza jambo la kushangaza kwa Simba katika mwanzo wa msimu huu, kwani ni mchezo wa tatu mfululizo ambao timu hiyo inamaliza ikiwa pungufu baada ya mchezaji wake kuonyeshwa kadi nyekundu.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar, Duchu alionyeshwa kadi nyekundu; mchezo wa pili dhidi ya Pamba Jiji, Jabaar alitolewa kwa kadi nyekundu, huku leo dhidi ya Singida Black Stars ikiwa ni zamu ya Anthony Mligo.

Licha ya changamoto hiyo, Simba imeonyesha uimara mkubwa kwa kushinda michezo yote mitatu ya mwanzo na kufikisha alama tisa kati ya tisa, jambo linaloiweka katika nafasi nzuri mwanzoni mwa mbio za ubingwa.

REKODI YA SIMBA BAADA YA MECHI TATU

🟥 Kagera Sugar vs Simba: Duchu
🟥 Pamba Jiji vs Simba: Jabaar
🟥 Singida Black Stars vs Simba: Anthony Mligo

12’ – Chama | Singida Black Stars 0-1 Simba
22’ – Sheikhan | Singida Black Stars 1-1 Simba
62’ – De Reuck (P) | Singida Black Stars 1-2 Simba
🟥 85’ – Mligo

FT: Singida Black Stars 1-2 Simba SC

 

Post a Comment

0 Comments