Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewashukuru wageni mbalimbali, wakiwemo mabalozi na viongozi waliofika kushuhudia hafla ya kuapishwa kwa Makamu wa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais Samia amesema uwepo wa wageni hao katika hafla hiyo ni ishara ya umuhimu wanaoupa Tanzania na mchakato wake wa kiuongozi.
Amesema tukio hilo limewapa fursa ya kujionea namna Katiba ya Tanzania inavyowezesha mabadiliko katika nafasi kubwa za uongozi kufanyika kwa utulivu na bila misukosuko.
Rais Samia amesisitiza kuwa utaratibu huo unaonesha umuhimu wa kuheshimu Katiba na taasisi za nchi, jambo ambalo linaendelea kuchangia utulivu na amani nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Rais Samia, mabadiliko katika uongozi yanaweza kufanyika kwa kufuata taratibu zilizowekwa kikatiba, bila kuathiri shughuli za Serikali na maisha ya wananchi.

0 Comments