RAIS SAMIA AMTAKA NDEJEMBI AJIFUNZE KWA WENGINE WALIOPITA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Makamu wa Rais mpya, Deogratius Ndejembi, kujifunza kutoka kwa viongozi waliowahi kushika nafasi hiyo kabla yake.

Rais Samia amesema ana imani kubwa na uwezo wa Ndejembi katika kutekeleza majukumu yake mapya na amemtaka kutumia uzoefu wa waliomtangulia katika kuimarisha utendaji wake.

Rais Samia ameyasema hayo leo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, baada ya kumuapisha Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amesema nafasi hiyo ni kubwa na yenye majukumu mazito, hivyo uzoefu na mafunzo kutoka kwa viongozi waliotangulia ni muhimu katika kumsaidia kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Post a Comment

0 Comments