RAIS SAMIA AZINDUA NYENZO ZA UTEKELEZAJI WA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 03 Agosti 2026 ameongoza hafla ya uzinduzi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.

 
HUPATI WATEJA!TANGAZA NASI SASA UPATE MAELFU YA WATEJA KWA ELFU TANO(5000) PIGA SASA 0654414804.

Hafla hiyo imewakutanisha viongozi mbalimbali wa Serikali, taasisi za umma na binafsi, wadau wa maendeleo pamoja na washirika wa maendeleo, kwa lengo la kushuhudia uzinduzi wa nyenzo zitakazotumika kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Nyenzo hizo zinatarajiwa kuwa mwongozo muhimu katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa ndani ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yanatekelezwa kwa ufanisi, uwazi na ushirikiano kati ya Serikali na wadau mbalimbali. Pia zinakusudia kuimarisha mipango ya maendeleo, ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati na matumizi bora ya rasilimali kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.

Kupitia uzinduzi huo, Serikali imeonesha dhamira ya kuendelea kujenga uchumi imara, kuongeza ushindani wa Taifa, kuimarisha utoaji wa huduma za kijamii na kuharakisha maendeleo yanayowanufaisha wananchi wote, sambamba na kuweka msingi wa Tanzania yenye uchumi shindani na ustawi wa watu ifikapo mwaka 2050.


 

Post a Comment

0 Comments