POLISI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAUAJI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limewafikisha mahakamani watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya Ferdinand Kefa Msakuzi (50), mkazi wa Majengo, Wilaya ya Sumbawanga.
 

Watuhumiwa hao ni Michael John Bubinza, aliyekuwa askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, na Spiliano Mmanyo Pascal, dereva wa bodaboda, wote wakiwa wakazi wa Sumbawanga.

Tukio hilo la mauaji liligundulika tarehe 28 Julai 2026, majira ya saa 6:00 mchana, katika Kijiji cha Kisumba, Wilaya ya Sumbawanga, ambapo mwili wa marehemu ulikutwa umetupwa vichakani.

Baada ya uchunguzi wa awali kukamilika, tarehe 19 Agosti 2026, watuhumiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Sumbawanga, ambako walisomewa shtaka la mauaji.

Post a Comment

0 Comments