MASHUA YA WAHAMIAJI YAPINDUKA,12 WAPOTEA

 Mashua iliyokuwa imewabeba wahamiaji imepinduka katika Pwani ya Kusini mwa Tunisia, na kusababisha vifo vya watu wawili huku wengine 12 wakiendelea kutafutwa baharini.

GUSA HAPA,NIMEBADILISHA MAISHA KWA KUUZA SOYA NA MAHARAGE MEKUNDU 

Mtu mmoja pekee amenusurika baada ya kuokolewa, huku vikosi vya uokoaji vikifanya msako wa kuwatafuta waliosalia.


Mashua hiyo iliondoka kati ya miji ya Zarzis na Ben Guerdane ikielekea Italia.

Tukio hilo linaongeza orodha ya ajali za wahamiaji wanaojaribu kuvuka Bahari ya Mediterania kuelekea Ulaya, licha ya juhudi za mamlaka za Tunisia na Umoja wa Ulaya kudhibiti uhamiaji usio rasmi.

Post a Comment

0 Comments