KIBAHA:ASKARI WAFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA GARI

 Askari wawili wa Jeshi la Polisi wamefariki dunia kufuatia ajali ya kugongwa na gari aina ya Toyota Noah wakati wakivuka kwenye kivuko cha waenda kwa miguu (zebra cross) eneo la Maili Moja, Wilayani Kibaha katika barabara kuu ya Dar es Salaam - Morogoro.

SOMA PIA,REJESHA HESHIMA YAKO CHUMBANI MWANAUME

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, ajali hiyo ilitokea Agosti 25, 2026 majira ya saa 1:40 usiku baada ya dereva Josia Isaya Arute (34) kuyapita magari mengine yaliyokuwa yamesimama na kuwagonga askari hao, ambapo Askari Izdory George Michael alifariki papo hapo huku Askari Rehema Juma Magawa akifariki asubuhi ya Agosti 26 akipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

Kufuatia ajali hiyo, dereva alikimbia eneo la tukio, lakini msako mkali ulioendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi ulifanikisha kukamatwa kwa gari hilo lililokuwa limefichwa eneo la Kwa Mfipa majira ya saa 2:40 usiku.

Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Tumbi kwa ajili ya taratibu za mazishi, huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani akisisitiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria dhidi ya madereva wazembe wanaokiuka sheria na alama za usalama barabarani.

Post a Comment

0 Comments