JELA MAISHA KWA KUMLAWITI MWENYE MATATIZO YA AFYA YA AKILI

 Imeandikwa na Ally Mandai.

Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Nestory Baro, amemhukumu Swaibu Issa Mpili (24), mkazi wa Kibugumo, kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana mwenye umri wa miaka 17, ambaye alikuwa na changamoto za afya ya akili.

Akisoma hukumu hiyo, Mhe. Baro amesema Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa na mashahidi katika kesi hiyo, na hivyo kuona kuwa mashtaka dhidi ya mshtakiwa yamethibitishwa.

Hakimu huyo amesema hu kumu hiyo imetolewa kwa kuzingatia sheria, kuhakikisha haki inatendeka na kuwa fundisho kwa watu wengine wanaoweza kujihusisha na vitendo vya aina hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kesi, Mpili alidaiwa kutenda kosa hilo katika eneo la Kibugumo, Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam, baada ya kumlaghai kijana huyo na kumpeleka nyumbani kwake.

Inadaiwa kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, Mpili alimtishia kijana huyo kwa kutumia kisu na kisha kumfanyia kitendo hicho kinyume na maumbile. Mahakama, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande husika, ilimkuta na hatia na kumhukumu kutumikia kifungo cha maisha jela.

Post a Comment

0 Comments