Kamati ya
bodi ya ligi pia imezikumbusha timu zote kuzingatia kikamilifu kanuni
ya 20 inayohusu matumizi ya Teknolojia ya Football Video Support System
(FVS), ikisisitiza kuwa mchezaji haruhusiwi kumlalamikia au kumshinikiza
mwamuzi kuomba marejeo ya matukio.
GUSA HAPA,UREJESHE HESHIMA CHUMANI NA TIBA LISHE
Kwa mujibu wa Kanuni ya
20(4), Kocha Mkuu au kiongozi mwingine wa juu kwenye benchi la ufundi
ndiye mwenye mamlaka ya kuwasilisha ombi la marejeo ya tukio katika
mfumo wa FVS, kupitia Mwamuzi wa Akiba.
Kanuni hiyo pia
inaelekeza kuwa iwapo mchezaji ataona tukio linahitaji marejeo ya FVS,
anatakiwa kumjulisha kocha mkuu au kiongozi wa benchi la ufundi kwa
ishara, ili kiongozi huyo awasilishe ombi hilo.
Kamati imeonya
kuwa ni marufuku kwa mchezaji kumlalamikia au kumshinikiza mwamuzi moja
kwa moja kwa lengo la kuomba marejeo ya FVS. Mchezaji atakayekiuka
masharti hayo ataadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62.
Kiongozi au Kocha pekee anatosha kuomba marejeo ya matukio kupitia FVS ?
0 Comments