Mtu mmoja ambaye bado hajatambulika, anayesadikiwa kuwa mkazi wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, amefariki dunia asubuhi ya leo, Agosti 4, 2026, baada ya kuanguka katika choo cha umma kilichopo Stendi Ndogo jijini Arusha.
GUSA HAPA,UMECHOKA KUTAFUTA MTOTO? TIBA LISHE HIZI ZITAKUPA TUMAINI JIPYA
Kwa mujibu wa mashuhuda, mwanaume huyo aliwasili katika stendi hiyo akitokea Dar es Salaam na alikuwa akijiandaa kupanda daladala kuelekea Monduli. Inadaiwa kuwa aliacha mzigo wake ndani ya daladala kabla ya kuelekea chooni.
Mashuhuda wamesema mwanaume huyo alionekana kuwa katika hali mbaya kiafya na alikuwa akitembea kwa shida. Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo walimsaidia kwa kumpatia fimbo ili aweze kufika chooni.
Inaelezwa kuwa baada ya kuingia chooni, alikaa kwa muda mrefu bila kutoka, jambo lililozua wasiwasi kwa watu waliokuwa eneo hilo. Baadaye mhudumu wa choo aliamua kufungua mlango ili kujua kilichokuwa kinaendelea.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, mhudumu wa choo amesema alimkuta mwanaume huyo akiwa ameinama ndani ya choo. Alijaribu kumtoa nje ili apatiwe msaada wa haraka, lakini muda mfupi baadaye mwanaume huyo alianguka na kufariki dunia.
Jeshi la Polisi linatarajiwa kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho pamoja na kuthibitisha utambulisho wa marehemu.

0 Comments