CCM YAMVULIA KOFIA RAIS DK. MWINYI KWA UTENDAJI MAKINI

Na Mwandishi  wetu,Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema kitahakikisha kila lililoahidiwa kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM  mwaka 2025-2030 yanatekelezwa  kwa wakati ,kwa viwango na ufanisi unaotegemewa.

Pia CCM imempongeza  Rais  wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuhimiza  ujenzi wa vituo vya kisasa vya mabasi yanayotumia nishati ya  Umeme.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati  Maalum ya NEC  zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis aliyesema kuanzia  huduma za usafiri wa  mabasi ya umeme, ni fakhari ilioje.

Mbeto aliutaja mradi huo utawapatia wananchi huduma za usafiri wa uhakika na  ubora,  katika namna ya kuboresha mfumo unaoipa haiba  mpya  mji wa Zanzibar.

Alisema lengo la Serikali  ya CCM ni kuhakikisha vyombo vya usafiri vinavyotoka maeneo ya  nje ya mji,  vinaishia katika vituo vya mabasi vitakavyojengwa pembezoni mwa mji.

"Yote yalioahidiwa katika ilani ya uchaguzi  ya CCM na ahadi za mgombea  urais yanatekelezwa.Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Wakoloni wameondoka na kuviacha visiwa vikiwa hohehahe kimaendeleo " Alisema Mbeto 

Aidha ,alisema chama cha CCM  kitaendelea kuikumbusha serikali yake na  kuhakikisha hakuna ahadi hata moja itakayoachwa pembeni.

Katibu  huyo Mwenzi alisema kwa taasisi  dhamana yoyote  itakayosimamia  uendeshaji wa usafiri huo mpya ,wafuate  utaratibu mpya wa utoaji  huduma za usafiri ili kutoa unafuu kwa wananchi.

"Katika usafirishaji lazima kuwe na utaratibu utakaowajali wazee, wagonjwa ,walemavu na  wanafunzi ili wasafiri kwa urahisi bila usumbufu"Alieleza .

Pia  mbeto amezitaka mamlaka zinazohusika na ujenzi wa miundombinu ya barabara,kuwa  makini katika kudhibiti uvamizi wa   hifadhi za barabara, ikiwemo ujenzi wa maduka na majengo mengine.

"Wananchi  wote wana wajibu wa kuendelea kuunga mkono utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuitunza .Mali ya umma ni mali ya kila raia hivyo lazima zilindwe na kutunzwa "Alisisitiza Mbeto


 

Post a Comment

0 Comments