KIHONGOSI: “MSISIKILIZE WANAOBEZA MAENDELEO YA SERIKALI”

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataka Watanzania kutowasikiliza wanasiasa wanaotumia majukwaa ya siasa kutoa matamshi ya kubeza na kupunguza thamani ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Kihongosi ametoa wito huo Mkoani Iringa wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi akiwa katika ziara yake ya kikazi ya kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi katika elimu, afya, maji na miundombinu, na matokeo yake yanaonekana kila mkoa lakini kuna baadhi ya wanasia wamekuwa wakitumia baadhi ya madhaifu machache kuwaaminisha kuwa hakuna kitu kilichofanywa na serikali.


 

Post a Comment

0 Comments