CCM: KONGOLE RAIS DKT. SAMIA KWA KUIPA HESHIMA TANZANIA KIMATAIFA


Na Mwandishi  Wetu,Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesifu uwezo, upeo,maarifa na ujasiri ulioonyeshwa na Mwenyekiti  wa CCM Rais Dk Samia Suluhu Hassan  kwa kulipa heshima Taifa wakati akijibu  maswali  katika ziara ya kiserikali nchini Urusi.

Kimeyataja majibu ya Rais Dkt Samia mbele  ya dunia , ni kudhihirisha kiwango cha uelewa  wake katika mawanda ya diplomasia  na utetezi wa maslahi ya Taifa.

Hayo yametamkwa  na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamis Mbeto Khamis , alipomzungumzia  Rais Dk Samia alipofafanua kutokuwepo kwa  vikwazo kwa nchi yake.

Mbeto  alisema akijibu swali aliloliita  la mtego ,Rais  alieleza   kinagaubaga nchi yake haijawekewa vikwazo na Taifa lolote duniani  na kwamba litabaki kuwa  mshirika  na Mataifa yote.

Alisema Rais akijibu kwa  utulivu, busara na hekima baada ya kuitaja  Tanzania haiko chini ya vikwazo na kwamba imekuwa ikihimiza ushirikiano na mataifa yote inagawaje haifungamani na Siasa za Taifa lolote.

"Tunampa mkono wa kulia wa hongera Rais  Dk Samia kwa upeo, maarifa kwa kuonesha kusimamia vema  kanuni  na misingi ya   diplomasia .Amelipa heshima  Taifa lake kwa usawa na manufaa ya pamoja.

Aidha Mbeto  alisema aina  ya majibu yake,  ndio msimamo wa Taiifa lolote linalojiamini, linalojitambua na linalotanguliza mbele maslahi ya nchi na watu wake.

"Majibu  baada ya swali aliloulizwa,  yakapokelewa kwa kushindo cha  makofi ya furaha   kutoka  kwa mwenyeji wake Rais  Vladimir Putin na Washiriki wa kongamano la  kimataifa la uwekezaji " Alisema Mbeto.

Mwenezi huyo  alisema Rais Dk Samia ameonesha kiwango cha busara, utulivu na umahiri wa kidiplomasia, hivyo amedhihirisha kuwa na ufahamu na  uliopevuka  kiutawala.

"Nchi yetu itabaki na msimamo wa kuongeza marafiki na Washrika waaminifu. Tanzania haitafuti maadui wala kuchagua kambi za migogoro ya dunia.Itajenga  dhima na kudumisha Urafiki, Biashara, Uwekezaji na  Ushirikiano"Alisema Mbeto.

Hata hivyo , Mwenezi  huyo alisema milango ya  Ushirikiano na  udugu wa miaka mingi baina ya Tanzania na Urusi , itaendelea kuwa wazi na kutanua wigo wa shughuli za Kiuchumi, Elimu, Historia na Uwekezaji .


 

Post a Comment

0 Comments