TAKUKURU YAENDELEA KUMSAKA ALEX MSAMA,DAU NONO LATANGAZWA

 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Kinondoni imesema inaendelea na msako wa Alex Msama ili ajibu mashtaka yanayomkabili

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam ijumaa, Mei 15, 2026, Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kinondoni, Elizabeth Mokiwa, amesema tangu watangaze kumtafuta bado hawajafanikiwa kumpata licha ya kutangaza donge nono kwa atakayefanikisha zoezi hilo.

Itakumbukwa, Januari 22, 2026 TAKUKURU ilitangaza kumtafuta ndugu Msama akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi, yakiwemo kuongoza genge la uhalifu, kughushi nyaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha.

"Jitihada za kumtafutia Alex msama bado zinaendelea na kuna dau kwa atakayefanikisha kumpata" amesema Elizabeth akijibu swali la mwandishi wa habari juu ya hatima ya suala hilo.


 

Post a Comment

0 Comments