Na Mwandishi Wetu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt.Eveline Munisi amefanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mei 18,2026 Jijini Dar es salaam akisisitiza dhamira ya Serikali kushirikiana katika kulinda maslahi ya wafanyakazi, waajiri na Taifa kwa ujumla.
Katika ziara hiyo, Dkt. Munisi alipendekeza maeneo matatu ya ushirikiano kati ya Serikali na NSSF ambayo ni kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu hifadhi ya jamii, kupanua wigo wa wanachama hususan katika sekta isiyo rasmi pamoja na kuimarisha huduma rafiki na za haraka kwa wanachama.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, Bw.Masha Mshomba amesema Skimu ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii imeendelea kuimarika kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo majengo ya biashara, makazi na Mradi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi uliotoa ajira zaidi ya 2,000.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

0 Comments