SABABU YA SIMBA SC KUWA KLABU BORA YA MWAKA BMT

 Na Ally Mandai.

Simba SC imetwaa tuzo ya Klabu Bora ya Wanaume wa mwaka katika Tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) 2025 zilizofanyika Jijini Dar es salaam huku mafanikio hayo yakidhihirisha mwendelezo wa ubora wa Klabu hiyo katika mashindano mbalimbali ya ndani na Kimataifa kwa mwaka 2025.

Tuzo hiyo imetolewa Mei 9, 2026 katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es salaam ambapo imekabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, na kupokewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Zubeda Sakuru mbele ya Wadau mbalimbali wa michezo Nchini.

Katika tuzo za Wanamichezo binafsi, Mwanariadha Alphonce Simbu ametwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kiume wa mwaka huku Stumai Abdallah wa JKT Queens na Timu ya Taifa ya Wanawake akitwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kike wa mwaka kutokana na mafanikio yao katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Kwa upande wa Vijana, Raymond Francis ametangazwa kuwa Mwanamichezo Bora Kijana wa Kiume wa mwaka huku Rose Kataboy akitwaa tuzo ya Mwanamichezo Bora Kijana wa Kike baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo yao kwa mwaka 2025.

Mbali na Wanamichezo, tuzo nyingine zilizotolewa ni pamoja na Kocha Bora wa Kiume aliyekwenda kwa Anthony Mwingereza, Kocha Bora wa Kike aliyotwaliwa na Esther Chabruma, Mwamuzi Bora wa Kiume aliyeshinda Shabani Mahobonya, Mwamuzi Bora wa Kike aliyokwenda kwa Dariso Mwidadi pamoja na tuzo za Wanahabari wa michezo zilizotwaliwa na Fatma Chikawe na Khalid Msabaha

Post a Comment

0 Comments