MHE. ANTONY MAVUNDE MGENI RASMI UZINDUZI WA KIWANDA CHA CHUMVI KILWA - LINDI

 
Wananchi na wadau mbalimbali wa sekta ya madini wanatarajiwa kushuhudia tukio muhimu la uzinduzi wa Kiwanda cha Chumvi litakalofanyika tarehe 29 Mei 2026 eneo la Lingaula, Kilwa – Lindi, huku Mhe. Antony Peter Mavunde, Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Mtumba, akitarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo muhimu.

Ujio wa Mhe. Mavunde ni ishara ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya madini, kuongeza thamani ya rasilimali za nchi na kufungua fursa za ajira kwa wananchi.

Hakika, uzinduzi huu ni hatua kubwa ya maendeleo ya kiuchumi na ukuaji wa viwanda nchini, hususan katika kuongeza thamani ya madini na bidhaa zinazotokana na rasilimali za Tanzania.

KARIBU TUSHUHUDIE HISTORIA YA MAENDELEO YA SEKTA YA MADINI TANZANIA 


 

Post a Comment

0 Comments