MBETO: KITUKO KUITAJA TANZANIA HAINA DEMOKRASIA NA UHURU WA KUABUDU

Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha Mapinduzi kimesema kwa namna yoyote kuihusisha Tanzania na Ubaguzi wa aina yoyote, au kudai inakiuka msingi ya demokrasia huku ikikandamiza uhuru wa kuabudu    ni kituko kipya kuwahi kutokea.

Aidha , CCM imesisitiza kuwa yeyote anayetoa madai hayo , haijui  historia ya kweli ya Tanzania  mbele  ya uso  wa dunia.

Matamshi hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum  ya NEC  Zanzibar , Idara ya Itikadi  ,Uenezi na Mafunzo,   Khamis Mbeto Khamis aliyesema wanaodhani watamudu kuipaka  matope Tanzania, wajitafakari zaidi. 

Mbeto alisema kama kuna Mataifa Duniani ambayo tokea yapate Uhuru wake yamekuwa yakiongozwa kwa kuheshimu Utawala wa Sheria, Kuenzi  Utu,  Haki za Binadamu na demokrasia, Tanzania ni miongoni  mwa Mataifa hayo.

Alisema kimsingi  na ukweli  usiopingika kwamba  Tanzania  si Mshrika wa mapenzi  ya jinsia moja,haishabikii ushoga na ubasha  pia haliwezi kuwa Taifa kibaraka lisilo na msimamo imara. 

" Tunaelewa kuwa ukitaka mbwa wako afe haraka mpe jina baya. Jaribio lolote la kutaka kuipaka matope Tanzania kwa namna yoyote ya kisingizio  cha uvunjaji wa Haki  za abinadamu  na demokrasia , madai hayo hayana  ushahidi wala   mashiko"  Mbeto. 

Alieleza kuwa hatua ya chama kimoja cha siasa   kususia Uchaguzi  Mkuu kwa sababu zao binafsi, kutaka kukinukisha na kukiwasha , hakuhalalishi kuthibitisha  madai ya kukosekana utawalabora, demokrasia au kufinya Uhuru wa watu kuabudu . 

"Tanzania ni Mwalimu Mkuu wa kufundisha  maana ya demokrasia ,utawalabora na kuenzi haki za binadamu Kusini mwa Jangwa la Sahara.Kama wapo wanaopaza sauti zao kwa shinikizo, mihemko na unazi,waache kufanya hivyo" Alieleza.

Pia Katibu huyo Mwenezi  aliongeza kusema  hakuna chama cha Siasa kilichozuiwa kisishiriki Uchaguzi Mkuu au kukamatwa kwa baadhi ya wanasiasa na kuwaweka ndani kimaonevu bila uvunjaji wa sheria  za nchi.

"Tanzania si koloni la Taifa lolote duniani. Limepata auhuru wake baada ya mapambano ya kisiasa yenye hoja na kuanza kujitawala. Tabia ya vitisho, ubabe na mikwala zikome toka sasa" Alifafanua.

Mbeto alisema iwapo kama kuna baadhi ya Mataifa yalitegemea kuutumia mwanya wa Uchaguzi  Mkuu ili Tanzania izame katika ghasia  ambazo  hatimae zingefanikisha Mapinduzi na  kuondoa utawala halali uliowekwa na wananchi, wakajipange upya.

"Hatuwezi kuishi kwa kupimana mbavu kila uchao. Waafrika wameshakataa aina yoyote  ya utumwa tokea enzi ya Ukoloni ukiwemo Utumwa  wa kudumazwa akili , maarifa na kushindwa kutoa maamuzi" Mbeto alisema kwa kujiamini.

Kadhalika akitoa mifano hai, Mwenezi  huyo alisema Tanzania ndio Taifa pekee  duniani lenye raia  ambao  wanoishi bila   kutobaguana kwa rangi,dini na kabila , badala yake  watu wake huheshimiana na kuishi kwa upendo. 


Post a Comment

0 Comments