MBETO AIPA HEKO SMZ KUPANDISHA MISHAHARA KIMA CHA CHINI

Na Mwandishi  wetu, Zanzibar  

Chama Cha Mapinduzi kimeipongeza kwa dhati SMZ  chini ya Rais wake Dk Hussein Ali  Mwinyi  kwa kupandisha mshahara   kima cha  chini kutoka laki 3 hadi laki 5.

CCM  kimeitaka SMZ  kuendelea mkakati wa  kutazama hali za maslahi ya  Wafanyakazi wa kima hicho  ili waweze kustawisha na kujijenga  kiuchumi .

MGANGA PROFESA BAHARI KISIKI ANAKUPA UTAJIRI MPAKA MILIONI 800 BILA MASHARTI

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati 
Maalum ya  NEC  Zanzibar ,Idara ya itikadi  ,Uenezi na Mafunzo,  Khamis mbeto Khamis mara baada ya smz kutangaza kima  kipya cha  mshahara visiwani humu


Mbeto alisema  ongezeko hilo la mshahara kwa kima cha chini ni fursa nyingine  kwa Wafanyakazi  kitakachosaidia katika kustawisha maisha yao.

Alisema kupanda  mshahara huo mpya  bila shaka smz imezingatia hali ya uchumi na maisha ya kila mzanzibari, garama za maisha na kuwapa motisha wafanyakazi,wazidi kusimamia majukumu yao kwa ufanisi.

'Siku zote motisha huongeza tija kazini. Tunawahimiza  Wafanyakazi  wote katika  taasisi  za umma,  Wizara ,Idara  na sekta zote  wakasimamie nidhamu  ya kazi ili kuongeza kasi ya  uzalishaji "Alisema Mbeto 

Aidha,alisifu uongozi  wa SMZ Awamu ya Nane kwa kujali na  kutazama na kuinua hali za wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji ahadi  za kisera na  ahadi binafsi za Rais.

"Tokea aingie madarakani  Rais Dk Mwinyi hii ni mara ya pili kupandisha mshara kima cha chini. Anafanya haya yote kwa kujali watu na maisha yao.Ungwana  wa mtu ni kutenda si kusema maneno matupu"Alieleza Mbeto 

Hata hivyo , Mwenezi  huyo alisema CCM kitaendelea kuzishauri mara kwa mara serikali zake ili zihakikishe maisha ya wananchi yanakimbizana na hali halisi ya kiuchumi.


 

Post a Comment

0 Comments