ALIYELIWA NA MAMBA KICHWA CHAKE CHAPATIKANA MTO WAMI


Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Rudewa, Athuman Salum (16), amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mamba akiwa katika shughuli za uvuvi kwenye Mto Wami uliopo wilayani Kilosa.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Kijiji cha Rudewa Batini na kuacha huzuni kubwa kwa familia, wanafunzi pamoja na wakazi wa kijiji hicho.

BOFYA HAPA MGANGA PROFESA BAHARI KISIKI ANAKUPA UTAJIRI MPAKA MILIONI 800  

 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Rudewa Batini, Masoud Msabaha, amesema kijana huyo alikuwa ameenda kuvua samaki mtoni kabla ya kushambuliwa ghafla na mnyama huyo hatari. 

 
Alieleza kuwa wananchi waliinua juhudi za kumtafuta marehemu mara baada ya tukio kutokea, lakini sehemu pekee iliyopatikana ni kichwa chake, ambacho tayari kimezikwa kwa taratibu za mazishi.

Baada ya tukio hilo, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Kilosa ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya, Shaka Hamdu Shaka, ilitembelea eneo la tukio na kuagiza kuwekwa kwa alama za tahadhari kuonyesha hatari ya uwepo wa mamba katika Mto huo.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi kuwa waangalifu wanapotumia au kuvuka mto huo, akieleza kuwa taarifa zilizopo zinaonyesha eneo hilo lina idadi kubwa ya mamba.


 

Post a Comment

0 Comments