FARIS BURUHANI AONGOZA VIJANA KONGAMANO LA TANZANIA KWANZA KAGERA

Uvccm Mkoa wa Kagera, Tanzania Kwanza.

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM katika mkoa wa Kagera Cde Faris Buruhani amewaongoza vijana kutoka wilaya zote huo kushiriki katika kongamano maalum la kuhamasisha amani lililoandaliwa na Chama cha Mapinduzi mkoa chini ya mwenyekiti wake Cde Dkt Nazir Karamagi na kuongozwa na mgeni rasmi Mhe Asia Halamga mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa na mbunge wa jimbo la Hanang aliyemwakilisha mlezi wa kichama wa mkoa huo Mhe waziri Mkuu dkt Mwigulu Nchemba. 

Katika hotuba yake Mhe Asia Halamga Ametaja bayana kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya CCM katika awamu ya sita Chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan na kusisitiza kuwa kila nchi ina demokrasia yake hivyo vijana wanapaswa kuchambua kwa makini na kuacha kasumba ya kufuata mkumbo huku akiwasisitiza wazazi kuhakikisha malezi bora kwa watoto ili kuepuka ongezeko la watoto wa wasio na makazi maalum jambo linaloweza kuhatarisha amani katika jamii.

Aidha Kongamano hilo limehusisha wataalamu watoa mada wakiwemo wataalamu kutoka makao makuu ya CCM, Wazee waasisi wa CCM, katibu wa CCM mkoa cde David Moreli, MNEC Karim Amri, karibu mwenezi wa CCM mkoa Cde Hamim Mahamudu n.k ambao wamewanoa vijana na wananchi walioshiriki kwa kutoa mada kemkem zenye mvuto na maarifa kama vile demokrasia, amani na usalama, siasa, uchumi, Historia ya chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na mambo makubwa yaliyofanywa na serikali yake kwa awamu sita mfululizo.

Tanzania kwanza
never again
CCM Kagera
Uvccm Kagera


 



Post a Comment

0 Comments