Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe Mosi Mei, Wakala wa Vipimo nchini umeendelea kuthamini mchango wa wafanyakazi wake kwa kuwatambua wale wanaofanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao.
Katika kuelekea maadhimisho hayo ya mwaka huu wa 2026, taasisi hiyo imemtambulisha rasmi Mfanyakazi Hodari wa Mwaka 2025/2026, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utendaji bora mahali pa kazi pamoja na kutambua mchango wa watumishi wanaosaidia kufanikisha malengo ya taasisi.
Kwa mujibu wa Wakala huo, tuzo hiyo hutolewa kwa mfanyakazi aliyeonyesha juhudi za kipekee, uwajibikaji, ubunifu pamoja na kujituma katika kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wananchi zinakuwa bora na zenye viwango vinavyotakiwa.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa inalenga kuongeza morali kwa wafanyakazi wengine kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku ikiakisi kaulimbiu ya kuthamini nguvu kazi ya watumishi katika maendeleo ya taasisi na taifa kwa ujumla.
Maadhimisho ya Mei Mosi duniani hutumika kutambua mchango wa wafanyakazi katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, sambamba na kuhimiza mazingira bora ya kazi na haki za wafanyakazi.

0 Comments