REFA MKENYA KUAMUA FAINALI YA SIMBA,YANGA MUUNGANO CUP 2026

 Na Ally Mandai

Mechi ya fainali ya Kombe la Muungano 2026 kati ya Wananchi, Young Africans SC dhidi ya Wekundu, Msimbazi, Simba SC itaamuliwa na mwamuzi Dickens Mimisa Nyagrowa kutoka Kenya ambaye atakuwa mwamuzi wa kati.

Mwamuzi msaidizi namba moja kwenye mechi hiyo ya Dabi ya Kariakoo ni Ali Mbwana kutoka Zanzibar huku mwamuzi msaidizi namba 2 akiwa Yusuph Shombe kutoka Zanzibar wakati mwamuzi wa akiba (4th offical) akiwa ni Is’haka Mwalile.

Mchezo huo utakaowakutanisha mahasimu hao wakubwa Nchini utapigwa leo Aprili 29, 2026 katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar majira ya saa 2:15 usiku.


 

Post a Comment

0 Comments