ONYO KALI:MAOFISA WATAKAOWAONEA WALIMU KUNG’OLEWA

Katika hatua inayotuma ujumbe mzito kwa sekta ya elimu, Waziri wa TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, ameonya kuwa hatasita kuwaondoa madarakani maafisa watakaobainika kuwanyanyasa au kutowahudumia walimu ipasavyo.

Akizungumza Aprili 17, 2026 wilayani Bahi, mkoani Dodoma kwenye hafla ya kuwapongeza walimu na wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa, Prof. Shemdoe alisema serikali inahitaji uwajibikaji wa haraka kwa masuala ya walimu. Alisisitiza kuwa kuchelewesha huduma ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.

Alitoa mfano wa mwalimu aliyesafiri zaidi ya kilomita 200 kufuata huduma inayopaswa kutolewa ndani ya dakika 10, lakini akaambiwa arudi siku nyingine hali aliyoiita “mzigo usiokubalika.”

Amesema serikali inalenga kuboresha mazingira ya walimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi, akionya kuwa yeyote atakayekwamisha juhudi hizo atachukuliwa hatua kali bila kusita.

Msisitizo wa uwajibikaji na huduma kwa wakati unaweka msingi mpya wa nidhamu na matokeo bora katika elimu nchini.



Post a Comment

0 Comments